Friday, March 18, 2011

Wakongwe wetu

Mafumu Bilali Bombenga na Yusufu Bernard wapiga Sax mahiri wenye uzoefu wa miaka zaidi ya 30

Shaaban Dede na King Kiki waimbaji na watunzi ambao wamekwisha tunga nyimbo nyingi maarufu.

Mzee Muhidin Gurumo na Mzee Said Mabela wakongwe wa msondo wamedumu katika sura ya muziki wa Tanzania toka miaka ya sitini bila kupotea

Hamza kalala mpiga solo na mtunzi aliyewahi kupitia bendi maaarufu kama UDA, Matimila, Vijana Jazz, Washirika Stars Bantu Group, pia ana wanae ambao nao wameanza kutoa mchango mkubwa katika muziki wa Tanzania

Mabrouk Khamis maarufu kama Babu Njenje, mwimbaji na mpiga drum wa Kilimanjaro Band, amekuweko katika anga la muziki toka mwishoni mwa miaka ya sitini. Bado sauti yake inaleta mchango mkubwa katika muziki wa Tanzania

King Kiki, Shaaban Dede, Bitchuka, Kabeya Badu majina ya waimbaji amabyo yamekuweko hewani zaidi ya miaka 30


Waziri Ally(Kisinger) na Abdul Salvador wapiga vinanda mahiri ambao wameweza kuweko katika fani kwa zaidi ya miaka 30, Abdul Salvador alianza kama mpiga gitaa akipigia bendi kama Biashara Jazz, na Bima Lee

No comments:

Post a Comment