Sunday, January 2, 2011

Mustafa Ngosha kuzikwa kesho Jumatatu


Mwanamuziki mpiga Bass wa DDC Mlimani Park Orchestra, ambaye alijulikana kwa jina maarufu la Ngosha atazikwa kesho saa 10 Magomeni. Ngosha alijiunga na DDC Mlimani Park miaka ya mwanzoni ya 90, akiwa anajulikana kama Charles John Ngosha, baadae alibadili dini na Kuslim na kupewa jina la Mustafa. Mwili wa marehemu umehifadhiwa Amana Hospital Ilala, na msiba utakuwa Magomeni katika maeneo ya kituo cha Bi Nyau, karibu na ukumbi wa DDC Magomeni. Kwa vile vikao vya kifamilia vinaendelea habari zaidi zitafuata

1 comment:

  1. Poleni sana kaka zangu wa Sikinde,tuko pamoja nanyi katika msiba huu mzito.Ngosha mwanamuziki
    aliyeheshimika sana kwa umahiri wake wa kupiga bass,tumempoteza mkongwe mwingine ambae hatasahaulika katika ulimmwengu wa muziki Tanzania na nchi za nje,kalale pahali pema peponi Ngosha"RESPECT"
    Abbu Omar,Prof.Jnr,(mwanamuziki)Japan.

    ReplyDelete