|
Picha za Jimi Hendrix ukutani ilikuwa ni muhimu |
|
Hapa yupo Mheshimiwa Balozi wetu mmoja ambaye pia alikuwa muimbaji mzuri sana wa nyimbo za Soul |
Kila zama katika miji kuna vijana wa aina mbalimbali
wanaotokana na aina ya malezi wanayolelelwa, mitaa wanayokulia, shule
wanazosomea na kadhalika. Palikuweko na makundi ya vijana wakiitwa
Mabrotherman, kutokana na kuiga utamaduni wavijana Wamarikani weusi. Mabrotherman, kwanza walikuwa wanatokana
na kundi la vijana ambao walikuwa wamepitia sekondari, walikuwa wakipenda
kusoma, kati ya stori muhimu katika vikao vya mabrotherman ni matukio toka
kwenye vitabu vya hadithi zilizoandikwa na Ian Fleming (James Bond) na James
Hadley Chas, na sinema ambazo zilitikisa kama vile Saturday Night Fever, au
filamu zote za Shaft, ama filamu zenye waigizaji weusi. Pia kusoma magazeti
kama Drum na Ebony. Mabrotherman walikuwa wasafi wenye kujipenda ambao Pamoja
na yote vijana walipenda sana kuparty, kwa kila kisingizio ilitengenezwa party
kulikuwa na party every week end. Vijana walichanga pesa na kukutana kwenye
nyumba mbalimbali, kuna wazazi walioruhusu vijana wao wafanye party katika
maeneo ya nyumba zao, wengine hata kuruhusu kutumia vifaa vya gharama wakati
huo kama music systems. Mavazi yakiwa Bellbottoms na slim fit
No comments:
Post a Comment