Tuesday, May 22, 2012

Mwanamuziki wa zamani John Mbula anaumwa anahitaji msaada


Waraka huu nimetumiwa na mwanamuziki mahiri Benno Villa Anthony.................Mkuu, kwanza kabisa namwomba Mwenyezi Mungu akujalie roho ya uvumilivu ktk kufuatilia taarifa hii. Itakumbukwa kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, nilikuwa na kipindi cha mahojiano na Manju wa muziki na mtangazaji wa TBC, komredi Masuud Masuud. Kwa vile kipindi kilirudiwarudiwa na huku Manju akitamka namba yangu ya simu, wengi waliinukuu, na kati ya hao walioinyaka ni Mzee John Mbulla, aliyekuwa mpiga sax wa Atomic Jazz. Mzee huyu kwa sasa kweli anaumwa sana. Zaidi ni maradhi ya macho, haoni. Kumbe kwao ni Mpwapwa ila kwa sasa anahifadhiwa na diwani wa Kibaigwa, Ndugu Richard Kapinye.......0717  303070. Baada ya kusikia kuwa wasanii wanachangiana ili kupata tiba, Diwani huyo alinipigia na nikazungumza nao wote wawili. Wameniomba nikupe taarifa hii ili uitoe kwenye vyombo vya habari, ikiwezekana apate msaada wa tiba. Diwani anasema kuwa John akipata operation ya macho atapona na kuanza kujitegemea maana nguvu bado anazo. KUMBUKA...Mzee John Mbulla ndiye aliyepiga Saxaphone kwenye wimbo wa "TANZANIA YETU NDIYO NCHI YA KUSIFIWA", wakati Mbaraka Mweshehe alipojiunga na Atomic Jazz  kwa muda..............Mkuu Kitime, Nina uhakika kama wana Media wakimtembelea na kutoa habari zake, naamini wengi wataguswa na kumsaidia.  Natanguliza shukrani zangu za awali. Asante Mkuu. 

2 comments:

  1. Dah Kaka,

    Umenikumbusha mbali.

    "...Leo nakupasulia ee, mpenzi wangu nikupendae,
    Usione ninatesekaa, ndiwe peke nikupendae.

    ...nduugu eee nihurumiee mwenzio ee ninatesekaa,
    Niisije nikapotea oooo niko mashakani.."


    We acha tu

    ReplyDelete
  2. Mzee John Mbula ni babu yangu baba yake mdogo na baba ni mim Yohana Mbula ni kweli kwa zamani ilikuwa wilaya ya mpwapwa lakini kwa Sasa tupo wilaya ya kongwa Kijiji Cha Ibwaga ndo tulipo kwa sasa

    ReplyDelete