Kassim Mponda alikuwa mmoja ya wapiga gitaa mahiri hapa Tanzania. Kama unakumbuka wimbo utunzi wa Kakere, wa Sogea Karibu uliopigwa na JUWATA ambao pia ulipambwa na kinanda cha Waziri Ally aka Kissinger, basi lile ndio solo la Kassim Mponda. Kwa kifupi alianzia Nyanyembe Jazz, akahamia Tabora Jazz,na kupitia Police Jazz Band Wana Vangavanga, Safari Trippers ,mbapo alihama na wenzie na kuanzisha Dar International, kisha akahamia Msondo, akapitia Shikamoo Jazz, hatimae mwanae akamnunulia vyombo akanzisha bendi yake mwenyewe Afriswezi. Mpaka mauti yake mwezi June 2002. Wanaoikumbuka Police Jazz, imekuwa nayo ni Band ya miaka mingi ambayo wanamuziki wengi maarufu walipitia huko,ni muhimu kuja kuongelea bendi za majeshi na mchango wake katika muziki wa Tanzania.
Ningependa kurekebisha kidogo hii report ya Mponnda. Kwanza kabisa Mponda hakupitia nyanyembe kwani wakati anaondoka yeye, Rashid hanzurunu na Omari kayanda nyanyembe ilikuwa bado haijaanza. Mponda alikhamia nyumba ya pili toka kwetu ili awe karibu na mjini, pia hall la Lumumba Bar walilokuwa wanapigia ni mpaka leo mali yetu. Nilikuwa na uhusiano wa kindugu na Mponda na hata wakati yuko polisi, Trippers pia Dar international. nilipoondoka kuja kusoma ujerumani nilisikia kaingia juwatta na mara ya mwisho kuonana nae ilikuwa dar legion alipokuwa na shikamoo Jazz. mimi pia nilishtushwa kusikia (miaka miwili) baada ya kifi chake kuwa ameshafariki. mungu amuweke pema. Kwa kuongeza tuu, Mponda alikuwa pia mahiri wa firimba mtindo wa kwela kama alivyokuwa arahamu mwinyishehe, lakini yeye alianza kupiga bass(TB Jazz) halafu Rhythm(western Jazz) na soloalianza akiwa polisi Jazz.
ReplyDeleteAksante sana kwa usahihisho, taarifa nyingi ni za mdomo na ni miaka mingi imepita hivyo hadithi huwa zinakosewa aksante sana kwa usahihisho.
ReplyDeleteNingependa kuongeza kidogo kwamba Mponda alipiga pia na DDC Mlimani Park mwishoni wa miaka ya 80....
ReplyDelete