Nimekuwa napewa changamoto kubwa kuhusu namna ya kusaidia wasanii wenzangu katika mapambano yao ya kupata haki kutokana na kazi zao mbalimbali walizorekodi au kushiriki. Hivyo basi nimeanzisha blog inayoitwa Wasanii wa Tanzania na Haki Zao ambapo patakuwa jukwaa la kutoa elimu kuhusu haki kama vile Hakimiliki, mikataba ya kazi mbalimbali, pia sehemu ya kupeana maoni na taarifa mbalimbali kuhusu biashara nataratibu nzima za shughuli za sanaa hapa nchini Tanzania. Nategemea wadau mtaweza kuchangia maoni na kuitangaza ili iwe kweli chombo muhimu kwa wasanii wa Tanzania.
No comments:
Post a Comment