THE JETS

THE JETS
THE JETS

PAKUA HII

Jumatano, 16 Mei 2018

THE RIFTERS BENDI ILIYOANZIA ILALA

Toka kushoto mstari wa nyuma Mlima, Adam Kingui, Dokta, Mbele kushoto, Nassoro 'Mick Jagger' Fadhil, Khalid Mosty

Bendi ya The Rifters ilikuwa ni bendi ya vijana wadogo ambayo ilianzishwa na Adam Kingui na James Mwinga huko Ilala Dar Es Salaam mwaka 1966. Ni bendi ambayo ilipitia mabadiliko mengi sana kwani katika miaka hiyo wanamuziki walikuwa wengi na kwa ujumla muziki kwa kundi kama hili haukuwa unalipa bali ilikuwa ni kwa upenzi wa muziki na pia wanamuziki wengi walikuwa pia shule. Adam alidumu kwenye bendi mpaka pale ilipokuja kufutika. 

Bendi ilianza na wanamuziki wafuatao, Mlima akiwa kwenye gitaa la rhythm, Mudi kwenye bezi, James Mwinga kwenye drums, baadae Mohamed Mdoe akajiunga kama mpiga bezi lakini akahamia kupiga drums. Raphael Sabuni akiwa anapiga gitaa la solo na rhythm.
Kadri miaka ilivyoenda Adam aliwaingiza wanamuziki wengine vijana kama akina Ebby Sykes, Nasolo "Mick Jagger" Fathil kwenye gitaa la bezi, Khalid Mosty kwenye drums na mwanamuziki toka Afrika ya Kusini Vuli Yeni, akiwa mwimbaji, wakati Belino nae aliingia kupiga gitaa la rhythm.
Mvulana mbele ni Jeff "Jifast", kwa sasa anapiga drums Sikinde. Bendi nyuma kule ni Rifters

Adam alikuwa akiaandaa maonyesho yaliyoitwa Tammi Shows pale Splendid Hotel, ambapo pamoja na muziki kulikuwa na wacheza show, jambo ambalo linapinga nadharia ya muda mrefu kuwa stage show zilianza baada ya safari ya Franco Tanzania mwaka 1973 Mwaka 1975 Adam Kingui na Nasolo Fathil waliondoka nchini na kuelekea Mombasa ambako waliendelea na shughuli za muziki. Shukrani kwa  Vuli Yeni kwa picha na habari.
The Rifters toka kushoto, Adam Kingui (lead guitar), Vuli Yeni (muimbaji), Ebby Sykes (gitaa la rhythm), Khalid Mosty(Drums),Nassoro ‘Mick Jagger’ Fadhili (Bass Guitar), wageni James Hadebe, wanne toka kushoto, Salum Mrisho ‘Choggy Sly’ wasita toka kushoto, Abdallah ‘Bob Dean’ Babu 


BAADA YA MAKALA HII KUONEKANA TUMEPATA PICHA ZA  KARIBUNI KABISA ZA NASSORO MICK JAGGER FADHILI..ASANTE SANA  ZOE GORDON-HUBER KWA PICHA HII. MZEE BADO YUMO KATIKA MUZIKI HUKO UJERUMANI
ZAMANI
LEO


Maoni 3 :

Bila jina alisema ...

lohh memory kubwa sana thanx

John Kitime alisema ...

THANK YOU ZOE

John Kitime alisema ...

The Rifters started at karikoo .ungoni street and playing at splendid hotel.independence avenue which Is now Samora.abdu on rhythm mohamed Mick Hager on bass Adam kingui on lead and vocals .unknown hafidh on drums there also playing in schools.....SALIM WILLIS