Saturday, October 22, 2011

Masafa Marefu na Tancut Almasi Orchestra




Kasaloo Kyanga ndie mtunzi wa kibao hiki maarufu, kilirekodiwa RTD Dar es Salaam katika awamu ya pili ya recording za Tancut Almasi. Recording hii ilitaka kuvunja bendi kwa kuwa wakati bendi ikiwa studio, Said Mabela alipita studio na Katibu wa bendi akamuuliza kwa siri anausikiaje muziki? Sijui kwa sababu gani lakini Mabela alijibu, "Hapa hakuna kitu nasikia solo tupu". Katibu wa bendi ambaye pia wakati huo alikuwa Katibu wa tawi la JUWATA la Tancut, akawajia juu wanamuziki wa Tancut kuwa wanapiga solo tupu na hivyo waache kurekodi bendi irudi Iringa kwa mazoezi zaidi. Ulikuwa ugomvi mkubwa, wakati huo Mabela amekwisha ondoka hata kumuuliza alikuwa ana maana gani haikuwezekana. Fundi wa RTD James Muhilu ndie aliyemtuliza Katibu huyo kuwa nae haelewi maana ya maneno ya Mabela na recording ikaendelea na dunia ikapata bahati ya kusikia kibao hiki.


Ninakwenda safari, safari yenyewe safari ya kikazi,
Ninakwenda safari, safari yenyewe ya masafa marefu,
Najua hapa utabaki, watasema mengi,
Pia wabaya wetu mama watafurahi.
Chorus
Safari sio kifo mama iyeeo
subiri ntarudi mama iyeoo


Nikirudi mama nipokee kwa mikono miwili
Nikirudi mama nitakuletea zawadi
Zawadi nono mama watototo
Iyee mama iyee



No comments:

Post a Comment